November 25, 2011

Mariah Yeater Ahojiwa kuhusu Jinsi Ilivyokuwa Wakati Akipewa Ujauzito Na Justin Bieber

Mwanamke anayefahamika kwa jina la Mariah Yeater aliyeibuka na kudai kwamba amezaa na Justin Bieber hivi karibuni amefanyiwa mahojiano na The Insider na kueleza jinsi ilivyokuwa wakati akikutana na Justin.

Na alipoulizwa kwanini usiku huo mabodyguard walikuwa mbali na Justin, akajibu "No comment." Pia, alikataa kusema kama ana vithibitisho gani vya kuwa mtoto wake ni wa Justin's. Na ikaonekana kwamba maelezo yake yana mapungufu mengi ndani yake!


Hivi katika hali ya kawaida tu, wewe kama shabiki wa JB au unamjua vizuri kijana huyu, unadhani ni kweli inawezekana kwamba anahusika na suala hili la kuzaa nje tena na mwanamke wa kupita tu huku akiwa yuko kwenye mahusiano na mrembo wa hadhi yake?


Katika taarifa nyingine zilizopatikana kutoka TMZ zimedai kwamba Justin Bieber sio mwanaume wa kwanza kusingiziwa mambo kama hayo na Mariah Yeater's.


Mwaka jana pia ilidaiwa kwamba mwanamke huyo alimsingizia ex-boyfriend wake aitwaye John Terranova kwamba ndiye aliyempa mimba ya mtoto huyo ambaye Justin anasingiziwa kwamba amemzalisha.


"TMZ walizungumza na Frances Lippe ... na kumuelezea Mariah Yeater kwamba alikuwa akitembea na mjukuu wake aitwaye  John Terranova huko Las Vegas muda mrefu wakati wakiwa high school.


Lippe amesema kwamba Yeater alienda nyumbani kwake December 2010 na kumwambia Terranova kwamba ana ujauzito wake. Lakini John alikataa na kumwambia kwamba hahusiki na ujauzito huo.


Wawili hao waliishi katika ugomvi na polisi wakaitwa kuja kuwasuluhisha ... kwasababu Maria alivunja kioo cha gari lililokuwa nje ya nyumba ya akina John.


Baadaye siku hiyo, kwa mujibu wa taarifa za polisi, Maria alirudi nyumbani kwao na kuanza kutafuta pesa kwaajili ya kununua kioo alichokivunja ... kisha akarudi tena kwa kina Terranova ... ambako alimpiga John vibao vitatu usoni kwa mkono wake.


Maria alikamatwa na kufunguliwa mashtaka ya kushambulia na kuharibu mali.  Na mpaka sasa kesi yake bado iko mahakamani huko Vegas.


Lippe akaeleza kwamba hawajawahi kuonana na Maria tena tangu mwezi   December mwaka jana. Miezi 10 baadaye, Mariah ametokea tena ... na sasa ameanza kumtuhumu Justin Bieber kwamba ndiye baba wa mtoto wake. Hata hivyo JB amekana tuhuma hizo na kudai kwamba yuko tayari kupima DNA yaana Vinasaba ili kuujua ukweli, katika taarifa za hivi karibuni Maria aliamua kufuta kesi juu ya Justin Bieber kumzalisha huku JB akisema atamfungulia mashtaka ya kumdhalilisha.


Mariah alijifungua mtoto wa kiume huko San Diego mnamo July 6 na chaajabu hakumtaja baba wa mtoto wake kwenye cheti cha kuzaliwa. "

No comments:

Post a Comment