November 25, 2011

Albam Mpya Ya Drake ‘Take Care’ Yatabiriwa Kufanya Mapinduzi Kimauzo Wiki Hii.

Mashabiki wa rapa Drake wameonesha uzalendo wa kuikubali albam yake. Albam ya Take Care ni ya pili kutoka kwa The Young Money star’ imeanza kuonesha dalili za kufanya vizuri  kwa wiki ya kwanza baada ya kuingia sokoni Nov 15.

Take Care, ambayo pia ilianza kupokea maoni ya kukubalika tangu mapema, kwa sasa iko katika mbio za kuelekea No. 1 katika chart za albam bora za Billboard Top 200 albums kuanzia wiki ijayo. Kwa mujibu wa HITS Daily Double, project hii inatabiriwa kuwa itauza nakala kuanzia 675,000 mpaka 725,000 kwa kulinganisha na mauzo ya siku ya kwanza ilipotinga sokoni.

Kiasi hicho kitampa Drizzy nafasi ya kuingia katika tatu bora ya mauzo akiwa nyuma ya Lady Gaga’s na albam yake ya Born This Way iliyouza nakala (1.1 million) akifuatiwa na Young Money boss Lil Wayne, ambaye albam yake ya Tha Carter IV ilifanikiwa kuuza nakala Milioni moja ndani ya wiki yake ya kwanza.

Na hii itakuwa albam ya kwanza kutoka kwa Drake’s kuuza mauzo makubwa kiasi hicho ikiwa ni ya pili kutoka ile ya Thank Me Later, ambayo iliingia sokoni na kuuza nakala 447,000 June 2010.

No comments:

Post a Comment