November 25, 2011

20 Percent abambwa na GANJA!

Jeshi la Polisi Wilaya ya Kilwa, mkoani Lindi, limemsweka nyuma ya nondo na kumfikisha kwa pilato (Mahakamani) msaani wa Bongo fleva, Abbas Hamisi Kisanza au kwa jina la kisanii 20%, kwa tuhuma za kupatikana na bangi.

20% alikutwa na zahma hilo alipokuwa ktk ziara ya kimuziki ktk mikoa ya Kusini, Lindi na Mtwara.

Inaelezwa msanii huyo akiwa kwenye gari aina a Toyota Nadia

 alisimamishwa na askari kwa ukaguzi wa kawaida ambapo katika zoezi hilo polisi walifanikiwa kubamba bangi kiasi cha gramu 20, ikiwa imehifadhiwa ndani ya droo ya gari hilo na kumfikisha kituoni.

Tayari msanii huyo wa Bongo fleva amefikishwa Mahakamani na kukana shitaka hilo. Tutaendelea kuwa update.

No comments:

Post a Comment