August 20, 2010

MWIMBAJI wa bongo fleva, Diamond, amesema atajitahidi kuelimisha jamii huku ikiitangaza mitaa ya Tandale na kuendeleza vipaji vya vijana wenzake.
 Diamond anayetamba na wimbo wa Mbagala, ni mkazi wa mitaa ya Tandale inayojulikana sana kwa vijana wake kujihusisha na kazi za hatari.


Akizungumza na Mtanzania Jumapili, kijana huyo aliyepata tuzo tatu mwaka huu, alisema kwa kufanya hivyo atafanikiwa kwa vitendo kuendeleza vijana wenzake. Alisema atakuwa akiandaa matamasha ya aina mbalimbali akianzia na kupiga vita malaria na mengineyo na kushirikisha wasanii wengi wa Tandale na sehemu nyingine za nchi.
“Maendeleo ya Tandale yataletwa na sisi wenyewe watu wa kule, maana ndio kwetu kabla ya kuanza kuwa na jina kama sasa baada ya kusota kutafuta mafanikio. “Naamini Mungu atanisaidia kwa kuhakikisha ninafanikiwa kwa vitendo kujiweka mahali pazuri mimi na wasanii wenzangu tunaoishi kwa ajili ya sanaa,” alisema.

No comments:

Post a Comment