August 21, 2010

Mauaji Ya Dereva Tax Mwanza Utata Mtupu.


Dreva mmoja wa taxi katika jiji la mwanza ameuawa baada ya kushambuliwa kwa kuchomwa visu shingoni na kichwani baada ya kukodiwa na watu wasiofahamika

 Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamemtaja dreva taxi aliyeuawa kuwa ni kaloli corneri mkazi wa mtaa wa karume nyamanoro jijini mwanza

Akithibitisha kuwepo kwa tukio hilo la mauaji kaimu kamanda wa polisi mkoa wa mwanza bwana mgetta jandwa amesema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia leo katika barabara ya makongoro. Marehemu kaloli ambaye alikuwa akiendesha gari aina toyota saloon lenye namba za usajili t406 bcx akiwa anaegesha katika mgahawa wa pizeria jirani na hotel ya new mwanza inadaiwa alikodiwa na watu ambao hawajafahamika kutoka baa ya villa park

Kwa mujibu wa kaimu kamanda wa polisi mkoa wa mwanza bwana jandwa wauaji baada ya kutenda unyama huo walitoweka huku wakiuacha mwili wa marehemu na gari lake katika eneo la tukio. Baadhi ya madreva taxi jijini mwanza wameelezea kushitushwa na mauaji ya kinyama ya mwenzao kaloli ambapo akizungumza kwa niaba ya wenzake dreva taxi evod rwambula amewataadharisha madreva taxi kuwa makini na wateja wao wa usiku na ikiwezekana wachukue wateja wanaowafahamu vizuri
POLISI WAKIFANYA TATHMINI USIKU WA TUKIO.
DREVA TAX MAARUFU WA MAENEO YA VILLA NA KISS CLUB JIJINI MWANZA AITWAE KAROLI (UMRI KATI YA 30-35 KABILA MUHAYA), MWENYE GARI TOYOTA PREMIO LENYE NAMBA ZA USAJILI T406BCX AMEUAWA KIKATILI NA MTU ASIYEJULIKANA KWA KUCHOMWA KISU SHINGONI NA BAADHI YA MAENEO KICHWANI.

No comments:

Post a Comment