August 20, 2010

Joh Makini In The Video Soon





KIBAO kipya cha mkali wa Hip Hop kutoka Kanda ya Kaskazini, Joh Makini, kiitwacho Karibu tena, kitatengenezewa video yake muda mfupi ujao.
Mwamba huyo wa Kaskazini, Joh, alisema jana kuwa baada ya kazi hiyo ambayo ilifanywa katika studio za B Hits kufanya vizuri redioni kwa zaidi ya mwezi mmoja na nusu, sasa ni zamu ya mashabiki kuiona katika televisheni.
“Nimeshazungumza na Visual Lab na wakati wowote tutaanza shooting. Katika kibao hiki nimemshirikisha dada mmoja anaitwa Fatma, dadake Hard Mad. Nadhani itasumbua kama nyimbo zangu nyingi zilivyofanya,” alisema. Joh Makini, mmoja wa wana Hip Hop wanaofanya vizuri nchini kwa sasa.
Amesema kibao hicho ni mwendelezo wa nyimbo anazotaraji kuwemo katika albamu yake ijayo ambayo inatayarishwa.

No comments:

Post a Comment