August 21, 2010

Mwisho Amaliza Adhabu Yake Mjengoni BBA 5

Mwakilishi wa Tanzania kwenye Jumba la Big Brother, Mwisho Mwampamba, ameelezea kufarijika baada ya kumaliza adhabu aliyopewa yeye pamoja na mshiriki wa Nigeria, Uti.
 Adhabu Hiyo Ilkuwa ya kuvaa suruali inayowaunganisha wawili hao kwa siku moja na nusu kutokana na vitendo vya vurugu na uharibifu walivyovifanya Jumapili iliyopita.



Mara baada ya shoo ya kutolewa mjengoni kwa mshiriki wa Angola Tatiana, washiriki walifanya vitendo vingi vya ajabu kutokana na pombe walizolewa.



Mwisho aling'oa mti uliopandwa kwenye chungu kilichopo bustanini na kumpiga nao Uti, ambaye naye aliuokota na kumtupia Mwisho, kabla ya Mwisho naye kwenda kuchukua 'fire extinguisher' ambalo ni maalum kwa ajili ya dharura ya kuzimia moto na kumpulizia Uti. Kutokana na vitendo hivyo, Biggie akatoa adhabu kwa wawili hao ya kuvaa suruali mbili ambazo mguu wa kila suruali moja umeunganishwa na suruali nyingine. Adhabu hiyo ikawafanya wawili hao kuambatana kila waendapo.



Sheria za Biggie katika adhabu hiyo iliyodumu kwa saa 36 ilikuwa wazi kwamba wawili hao walitakiwa kuoga pamoja, kulala pamoja, na kama mmoja alihitaji kwenda chooni, mwingine alitakiwa kumshikia mwenzake mlango.



Kwa kufungwa pamoja, wawili hao waliingia pamoja kwenye chumba cha faragha cha mahojiano na Biggie na walifanya "jukumu" la wiki pamoja. Wawili hao walionekana kutofautiana wakati wote, kutokana na Uti kumkasirikia Mwisho akimtuhumu kuwa ndiye chanzo cha wao kufungwa pamoja. Uti alimuita Mwisho kwa majina yote ya hasira kama "nyani wa kihistoria", "sokwe" na "mpuuzi". Mwisho alijibu na kusema mambo mengine ni magumu mno kwa Uti kuyaelewa.



Na hata walipokuwa wakifanya "jukumu" la wiki walilopewa na Biggie, wawili hao walikuwa hawaafikiani kirahisi.
Uti alikuwa akikasirika na kila mara na kumwambia Mwisho kuwa arejee kwa Meryl ili na yeye aende kwa Sheila kwani amemmisi sana.



Meryl anajificha kwa Mwisho
Muda mfupi baada ya kufanya mazoezi, Meryl wa Namibia alimweleza Sheila wa Kenya kuhusu Yacob (Ethiopia) alivyojaribu kumuweka Munya (Zimbabwe) katika upande wake baada ya uhasama wao. Sheila alimweleza Meryl kuwa Yacob alifadhaishwa na kitendo cha kupigiwa kura na washiriki wenzake kuingia kwenye chekeche la kutolewa mjengoni, lakini kijana huyo wa Ethiopia alijichimbia mwenyewe kaburi lake kutokana na kukorofishana na washiriki wenzake wengi ikiwa ni pamoja na kuwaomba mwenyewe wampigie kura ya kutolewa mjengoni.

Jumanne, Yacob na Meryl walibwatukiana vikali ambapo Yacob alimtuhumu Meryl kuwa yuko na Mwisho kwa sababu tu Munya alimtema na kwenda kumuopoa Tatiana. Hata hivyo, Munya alimpoza Meryl kuwa asijali yale anayoambiwa na Yacob.






No comments:

Post a Comment