October 18, 2010

New Era Music:

Producer Duke ameamua kuwaweka (karibia) vijana wake wote kwenye nyimbo moja ambayo imesimama (ipo chini hapo). Kuanzia mwanzo hadi mwisho sijaona kasoro; flow ni kali, mistari imetulia. Na muhimukuliko yote, wana punch line delivery ambayo inaenda sambamba na beat.
 
Bila shaka hawa vijana wako makini sana — nasema hivi kwasababu kuna metaphors (za kitaa) nyingi sana ambazo zitakuacha unatabasamu, unacheka au kufikiria.
Ukiacha hayo, mara nyingi wasanii wengi hutegemea beat nzuri ili iwabebe. Kwenye huu wimbo wao, beat ni kali sana (Duke kajipinda!), ila kwa mtazamo wangu nadhani vijana wake wamemfunika kwa ushairi.

Nimepata moto wa kuandika makala kuhusu hawa vijana ili kuwapa moyo, na kuwasihi waendelee hivyo hivyo. Watafika mbali…

No comments:

Post a Comment