October 19, 2010

Genevieve aanza vibaya:

Mrembo wa Tanzania anayeshiriki mashindano ya Miss World yatakayofanyika kwenye mji wa Sanya, kusini mwa China, Genenivive Mpangala ameshindwa kuingia kwenye 40 bora ya shindano la vazi la ufukweni. Shindano la vazi la ufukweni lilifanyika juzi usiku na warembo 40 walichaguliwa kati ya 120 huku Mrembo wa Bahamas, Brakena Bassett akitajwa kuwa amefanya vizuri katika shindano hilo la Miss World Beach Beauty (Best Body Swimsuit) lililokuwa la aina yake.

Mrembo huyo anatarajia kupata tuzo yake siku ya shindano la Oktoba 30 kwenye mji wa Sanya. Braneka pia alionekana kwenye vipindi vya televisheni vya Janice Dickinson Modelling Shown mjini Los Angeles nchini Marekani.

Katika hatua nyingine, Miss Botswana, Emma Wareus ametajwa kuwa mmoja wa warembo wanaotarajia kutwaa taji la dunia nchini China, kwa mujibu wa wabashiri wa mambo.

Mrembo huyo ni kati ya warembo wanaotokea Ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara na kwa mujibu wa Shirika la Habari la OLBG, Wareus anapewa nafasi kubwa kutwaa taji.

'Kamilla Salgado, Miss Brazil anafuatia katika ubashiri kisha Miss Colombia Laura Restrepo anayetajwa kuwa na nafasi.

"Warembo wanaotajwa na kuunganisha washindi ni Miss Botswana Emma Wareus na Miss India, Manasvi Mamgai ambao wote wanalingana kwa pointi," lilisema OLBG.

Wareus amekuwa kivutio kutokana na uzuri wake pamoja na mambo anayofanya.

Warembo wengine wanaotajwa kuwa wanaweza kufanya vizuri katika ngazi ya Afrika ni Miss Zimbabwe, Samantha Tshuma, Miss Angola, Ivaniltan Jones na Zindaba Hanzala kutoka Zambia. Pia Nicole Flint wa Afrika Kusini na Odile Gertze kutoka Namibia, Ella Kabambe wa Malawi na Karabeho Mokoallo anayetoka Lesotho.

No comments:

Post a Comment