October 26, 2010

Mandojo Yuko Behind Bars:

Ipo stori inayovuma kwamba mchizi aliyewadatisha wabongo ngoma ‘Nikupe Nini’ a.k.a ‘Kanikamulie maji ya ndimu nina kiu koma’,
Joseph Michael ‘Mandojo’ yupo nyuma ya nondo Singida...nikimaanisha 'Jela'.

Kwa mujibu wa source mbalimbali ziliwasiliana nasi ni kwamba msanii huyo amefungwa miaka miwili jela lakini haijabainika ni kisa gani ambacho kimempeleka ubayani.

Mshirika wa Mandojo, Precioust Juma ‘Domokaya’ last week alibainisha ya kuwa hata yeye ishu hiyo bado hajaipata fresh, anachojua ni kwamba mchizi yuko nyumbani kwao Manyoni, Singida kwa ajili ya matatizo ya kifamilia likiwemo lile la kufiwa na baba yake mzazi. “Mi pia sijui chochote kuhusu hilo kwa sababu sijapata simu au taarifa yoyote kutoka huko, siwezi kulizungumzia hilo sana,” alisema Domo.

Tangu wiki iliyopita habari zimekuwa zikizagaa jijini kuwa mchizi huyo ametupwa lupango kwa miaka 2.

Hata hivyo wasanii mbalimbali wakubwa pia walimwaga data kwamba Mandojo ameingia kifungoni kwa kosa la kupigana na washkaji wengine wa pande hizo.

Meza yetu inaendelea kufwatilia kwa makini habari za bingwa huyu na itakuwa ikiku-update kila inapopokea habari mpya.

No comments:

Post a Comment