Kanye West na Nicki Minaj wanaongoza katika chati, Lakini je ni katika level ya Gold Sales? Lil Wayne na Kid Cudi wamefanikiwa kufika level ya Gold Sales, huku Lloyd Banks akiwa ameng’ang’ania katika 25 Bora,
Curren$y, Yelawolf na Ne-Yo wote wakiwa katika nafasi moja.Wiki ya kufurahisha zaidi katika chati za muziki duniani imejidhihirisha katika mwezi huu. Kama wengi walivyotabiri, Kanye West anaongoza katika chati akiwa na albam yake ya tano ya My Beautful Dark Twisted Fantasy.
Albam ambayo kwa kiasi kikubwa ilipewa promo kubwa na siku maalumu aliyoitenga mwenyewe katika kuachia ngoma mpya kila ijumaa na kuiita siku hyiyo kama "G.O.O.D. Friday" ambayo imesaidia kuweza kukaribia kupata Gold Sales katika mauzo yake ya wiki ya kwanza ambapo iliweza kuuza zaidi ya nakala 497,000.
Mtandao Amazon ulikuwa ukiipromoti albam ya Kanye West kwa Digital Download iliyowapa nafasi mashabiki kuidownload kwa gharama ya dollar tano kwa muda wa wiki nzima.
Ukimzungumzia Nicki Minaj, albam yake ya kwanza imeshika nafasi ya 2 katika chati hizo. Ikiifuatia albam ya Lil Wayne “Im Not A Human Being” kutoka Young Money Cash Money Records, ambayo imeweza kuuza nakala 375,000 za Pink Friday. Katika albam hii amewashirikisha wasanii wanaoimba na wanaofoka wakiwemo will.i.am, Drake na Eminem.
Baiskeli iliyoundwa na Kampuni ya Def Jam kwa wasanii wa RnB na Pop ambao ni Rihanna na Ne-Yo bado wanaijaza vizuri Top 10. Katika wiki yake ya pili RiRi a.k.a Rihanna na project yake ya Loud anaendelea kuganda katika nafasi ya 6 kwenye main stream, akiwa amewapa collabo Drake, Eminem na mwanadashori Nicki Minaj.
Kwa upande wa “Nice Looks” Ne-Yo, albam yake ya Libra Scale inashika nafasi ya 9 katika chati. Idea ya albam hii imebase zaidi katika kitabu cha hadithi za watoto na shujaa anayeanguka katika mapenzi. Ne-Yo pia ametoa video ambayo inazidi kufanya ujumbe wa muziki katika albam hiyo uzidi kuvutia zaidi.
Albam ya Eminem imeruka nafasi mbili chini mpaka nafasi ya 24 wiki hii. Japokuwa mpaka sasa inakuwa ni albam pekee yenye mauzo makubwa mpaka kufika Triple-Platinum, katika wiki hii pekee imeuza nakala 48,000
Katika chati ifuatayo ya mauzo ya albam mbali mbali imefanyiwa makadirio ya karibu ya mara elfu moja kwa kili nakala.
Zifuatazo ni albam zilizoingia Top 5 katika chati ya albam 200 Bora za Hip Hop na RnB
1
Kanye West
My Beautiful Dark Twisted Fantasy
496,000
497,000
2
Nicki Minaj
Pink Friday 375,000
376,000
6
Rihanna
Loud
141,000
348,000
9
Ne-Yo
Libra Scale
112,000
113,000
24
Eminem
Recovery
48,000
3,053,000
Akiwa ameridhia kurudi upya kwa kundi la G Unit kwa wengi, albam ya tatu kutoka kwa Lloyd Banks, H.F.M. 2 (The Hunger For More 2) imeweka alama nzuri ya ujio wa lebo mpya ya kusambaza kazi za wasanii ya EMI Records. Akiwa na single iliyofika kiwango cha Gold na profile ya juu ya kufanya kazi na wasanii wakubwa kama Kanye West, 50 Cent, Raekwon na Eminem (katika toleo la mtandao wa iTunes), Lloyd Banks' hakusita kusema kuwa mauzo ya albam hiyo yamefeli ambapo katika wiki ya kwanza imeuza nakala 50,000.
Lil Wayne naye ameweza kujinyakulia medali ya dhahabu wiki iliyopita akiwa na albam yake ya I Am Not A Human Being. Albam hii ilikuwa katika mtindo wa Digital pekee katika kipindi chote alichokuwa jela na ilikuja kuwekwa katika CD baada ya kuachiwa huru. Hii inakuwa albam ya pili kushinda medali ya dhahabu kutoka kwa Weezy F Baby iliyotoka mwaka huu katika msimu wa majira ya baridi.
Currensy ambaye pia ni rafiki wa karibu wa Rapa Lil Wayne naye ameachia albam yake ya pili iitwayo Pilot Talk II, iliyotoka chini ya usimamizi wa Damon Dash na Kusambazwa na Def Jam huku ikiwashirikisha wasanii Raekwon na Spitta's ambaye alikuwa member wa zamani wa lebo ya No Limit.
Gasden, Alabama's Yelawolf naye ameingia katika mainstream ya albam zilizomo katika chati ya Top 200 akiwa na mixtape yake anayoisambaza kwa kutozingatia faida zaidi iitwayo Trunk Muzik 0-60. Kwasasa jamaa amesaini mkataba na kampuni ya Interscope Records.
Mwisho kabisa, ni albam nyingine iliyopata medali ya dhahabu ni kutoka Kid Cudi rapa kutoka Cleveland, Ohio iliyotoka mwaka 2009, Man Of The Moon: The End Of Day iliyouza nakala 500,000 na kubaki katika chati kwa muda wa mwaka mzima. Project hii imewashikisha Kanye West, Common na Chip Tha Ripper.
Mwendelezo wa mauzo ya albam nyingine zilizomo katika chati ni kama ifuatavyo.
25
Lloyd Banks
H.M.F.2 (The Hunger For More 2)
44,000
45,000
29
Lil Wayne
I Am Not A Human Being
37,000
511,000
83
Curren$y
Pilot Talk II
14,000
15,000
164 Yelawolf
Trunk Muzik 0-60
5,000
5,100
176
Kid Cudi
Man On The Moon: The End of Day
4,600
502,000
Je kundi la Black Eyed Peas, Flo Rida na Soulja Boy wataweza kuja kuisafisha chati hii na albam zao katika wiki mainstream ya wiki ijayo? Hili linabakia kuwa swali la wiki. Stay tuned kwa taarifa zaidi cheki nami next wiki.
No comments:
Post a Comment