November 29, 2010

yptian ready kwa makamuzi!

Msanii wa kimataifa ambaye ni mzaliwa wa Jamaica, Windel Beneto Edwards, maarufu kama Gyptian, amekwisha timba ndani ya Bongo na kuwaomba wanachuo na wapenzi wa muziki kujitokeza kwa wingi Jumamosi hii, katika Tamasha la ‘Music Str8Muzik Festival Inter-College Special 2010’ ambako amepania kufanya show ya kufa mtu.

Tamasha hilo litafanyika kwenye viwanja vya Posta Kijitonyama, jijini Dar es Salaam.

Gyptian alitua nchini juzi usiku na kupokewa kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam na Meneja Msaidizi wa SM, Isamba Kasaka.

Alisema kuwa amefarijika kufika Bongo katika tamasha la Str8Muzik Inter-College Special 2010, ambalo linakutanisha wanachuo kutoka vyuo na taasisi mbalimbali za elimu ya juu, kwa lengo la kubadilishana mawazo na kuburudika.

“Mimi nimeishafika na wasanii wengine wakubwa wapo njiani, sasa basi cha msingi ni watu wajitokeze kwa wingi kwa ajili ya tamasha hilo,” alisema Gyptian ambaye anatamba na nyimbo zenye miondoko ya reggae.

Gyptian alisema kuwa hii ni mara yake ya tatu kufika Afrika, kwani alishawahi kutumbuiza nchini Kenya na Senegal.

Wimbo wake wa kwanza, ‘Serious Times’ ulipata tuzo katika kipengele cha ‘Nyimbo Muhimu mwaka 2005’.

Miongoni mwa nyimbo nyingine ambazo zimemweka Gyptian juu katika ramani ya muziki duniani ni ‘Is There a Place’, ‘Beautiful Lady’, ‘Mama’ na ‘Don’t Cry’.

Aidha, msanii huyu katika nyimbo alizotoa hivi karibuni, amemshirikisha rapa mwanadada kutoka Marekani anayekuja juu, Nicky Minaj.

Wasanii wengine wa kimataifa wanaotarajiwa kuwasili leo kwa ajili ya Str8Muzik Festival Inter-College Special 2010 ni Elephant Man, Mims na T-Pain.

No comments:

Post a Comment