February 27, 2012

Joh Makini Ataja Nyimbo Mpya Atakazo Achia Baada Ya “Bye Bye”


Baada ya single ya bye bye kufanya poa toka aiachie miezi saba iliyopita, mwamba wa kaskazini rapper Joh Makini ametangaza exclusive kwenye millardayo.com kwamba sasa imefika time ya kuachia hit nyingine.


Amesema “nina track mbili ambapo moja kati ya hizo nadhani ndio itatangulia audio, moja inaitwa baby mama nimefanya na Belle 9 na nyingine inaitwa MANUVA nimefanya na producer Dunga, track ambayo nilikua nataka utangulie kama VIDEO bado nasubiri kufanyiwa kazi na Marco Chali kwa hiyo unanislow down kwenye mipango yangu, nadhani anabanwa na mipango yake atakapoimaliza nitaitoa hiyo video, nimeirekodi toka mwaka jana mwishoni “

Joh ameamplfy zaidi kwamba “nilitarajia mwezi huu wa february niachie video ya KIUTU UZIMA lakini inabidi nisubiri Marco chali amalizie, hizi nyingine ziko kwenye hatua za mwisho tu kwa sababu hata Dunga kasafiri anarudi leo nadhani mwishoni mwa wiki Manuva inaweza kuwa tayari, Baby Mama iko tayari naipitia tu studio ni Beat ya Nah Real, Voco nimefanya kwa Moner Gangsta, na nitaipitisha pia kwa Hermy B kwa ajili ya Mastering, chorus nimemshirikisha Dunga”

No comments:

Post a Comment