May 06, 2012

Diamond Atoa Msaada Kwa Watoto Yatima


Msanii ambae sasa hivi ndio anaongoza kwa kupiga show nyingi na zenye pesa ndefu, Diamond Platnums ametumia zaidi ya shilingi milioni mbili kutoa msaada wa vitu mbalimbali katika kituo cha kulelea watoto yatima Kinondoni Ananasif Dar es salaam.


Alipozungumza na FIXED 20 Diamond amesema hii sio mara ya kwanza anatoa msaada, huwa ni mara nyingi tu na huwa hatangazi kwa sababu dini ya kiislamu haifundhishi hivyo ila leo kafanya hivyo kwa sababu anataka kuhamasisha watu wengine kufanya hivyo.

Diamond amesema kwamba sehemu ya pesa aliyoitumia kutoa huo msaada huo ni kutoka kwenye show ya Mbagala Darlive aliyoshuka kwenye Helkopta pamoja na pesa aliyoipata kwenye tangazo la TV na RADIO alilolifanya hivi karibuni ambalo limemlipa zaidi ya shilingi milioni hamsini.

No comments:

Post a Comment